Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Mapigano yazuka upya Kivu Kaskazini

Mapigano Makali Yanaendelea Vikosi Vya Serikali Na Waasi Wa M23 DRC: Mapigano yazuka upya Kivu Kaskazini

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tangu mapema Alhamisi, Desemba 7, mapigano makali yamekuwa yakihusisha jeshi la Kongo dhidi ya waasi wa M23 katika maeneo kadhaa: Mushaki, Kilolirwe na Sake katika eneo la Masisi (Kivu Kaskazini).

Tangu saa 2 asubuhi (saa za Afrika ya Kati), milipuko imekuwa ikisikika katika eneo lote la Ruvunda na Rumeneti, takriban kilomita 3 hadi 6 kutoka Mushaki, na pia Kabati kwenye barabara ya Kilolirwe, takriban kilomita 15 kutoka Sake.

Siku ya Jumatano, mashambulizi ya anga ya jeshi la Kongo iliripotiwa katika maeneo ya waasi.

Vyanzo kadhaa vya ndani, vikinukuliwa na Radio Okapi siku ya Alhamisi asubuhi, vinaeleza kuwa ni jaribio la waasi wa M23 kutaka kudhibiti Mushaki, wakipitia vilima vya Ruvunda na Kabati, ambapo jeshi la Kongo lilijibu. wakazi wa eneo hili wametoroka makazi yao.

Wanabainisha kuwa wanamgambo wanaunga mkono jeshi la FARDC pia wameingilia kati mapigano haya.

Tangu saa 12 asubuhi kwa saa za ndani, jeshi limeripotiwa kutumia silaha zake nzito zilizowekwa karibu na Sake ili kumdhibiti adui mbali jiji hili.

Hata hivyo hadi majira ya saa kumi na mbili asubuhi hali ilikuwa ya kutatanisha, kiasi kwamba ilikuwa vigumu kujua ni nani hasa anadhibiti Mushaki. Hadi wakati huo, kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mapigano bado yalikuwa yakiendelea.

Waasi hao wanasemekana kufanikiwa kuteka mlima, unaojulikana kama "Antenne de Mushaki", katikati mwa jiji umbali wa kilomita 2 tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live