Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Mamia ya raia wakimbia makazi yao uvamizi wa M23

Kiongozi Wa Upinzani Ufaransa Akemea Kundi La M23 DRC: Mamia ya raia wakimbia makazi yao uvamizi wa M23

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati huu waasi wa M23 wakiendelea kujaribu kuchuka vijiji zaidi jimboni Kivu Kaskazini, mamia ya raia kutoka kwenye miji ya Kanyabayonga, Kayina, Kirumba na Mighobwe, wanakimbilia Lubero kutafuta hifadhi kutokana na mapigano.

Kwa mujibu wa mashirika kadhaa ya kiraia, mapigano mapya yaliripotiwa kwenye eneo la Kaseghe, ambako jeshi la Seriali na waasi hao wanawania kuudhibiti mji wa Mbingi kusini mwa Lubero.

Jeshi la Serikali FARDC linalosaidiwa na wapiganaji wa kundi la Wazalendo, wamekuwa wakijaribu kuwadhibiti waasi wa M23 kusogea katika mji wa Alimbongo kwenye barabara ya Kirumba-Butembo.

Ripoti iliyochapishwa na tovuti ya redio ya uloja wa Mataifa nchini DRC, Radio Okapi, imesema mashirika ya kiraia yameripoti waasi hao kuongeza nguvu kwa wapiganaji na magari ya kijeshi katika ĂȘneo la Mbingi.

Hata hivyo vynzo vya usalama kwenye maeneo hayo, vimeripoti hali ya utulivu kurejea wakatik huu Serikali ya Kinshasa ikiapa kukabiliana na waasi hao wanaodaiwa kusaidiwa na Serikali ya Rwanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live