Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Mafuriko yaua 28,000 kuhama makazi yao

Bandari Kelemn DRC.png DRC: Mafuriko yaua 28,000 kuhama makazi yao

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini DRC, serikali ya mkoa wa Tanganyika, kusini mashariki mwa nchi hatimaye inazungumza kuhusu maafa ya asili yanayoukumba mji wa Kalemie. Kwa mujibu wa waziri wa masuala ya kibinadamu wa mkoa huo, kaya 28,000 zilizopoteza makazi zimeathiriwa na kuongezeka kwa maji ya Ziwa Tanganyika zimetambuliwa. Anahakikisha kwamba serikali tayari imewapatishia hifadhi.

Waathiriwa wengine walihamia katika kijiji cha Katanika, magharibi mwa Kalemie. Baadhi wamejenga makazi ya muda, wengine wanaishi na familia zilizowapokea na kuwapa hifadhi. Hivi sasa, familia 28,000 zimehamishwa na janga hili. Dieudonné Kabulo, kiongozi wa Tume ya kitaifa ya haki za binadamu, CNDH huko Kalemie anasema kuna dharura.

Maafa kama haya yanapotokea, ni Serikali ambayo inapaswa kuchukua hatua ili kukabiliana nayo na sio raia. Ni lazima iwahudumie wahanga, ikibidi hata kujenga kambi ya waliohama maana inakuwa janga.

Kwa upande wake, Bob Morisho, waziri wa mkoa wa masuala ya kibinadamu, amesema maeneo ya kuwahifadhi watu hao, yamepatikana na kwamba mazungumzo yanaendelea ili kuwaandalia misaada.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live