Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Kwa nini televisheni ya 'Moise Katumbi' imeadhibiwa

Moses Katumbi.jpeg DRC: Kwa nini televisheni ya 'Moise Katumbi' imeadhibiwa

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja ya habari zilizozungumzwa sana tangu Krismasi nchini DR Congo ni pale ambapo jeshi la nchi hiyo liliposema kuwa limeiadhibu Televisheni ya Nyota na magazeti mengine kutokana na habari "kuvuruga, kuvunja moyo na kugawanya jeshi".

Katika taarifa yake, msemaji wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alisoma kwa makini sana anachokisema, Jenerali Meja Sylvain Ekenge alisema kuwa siku za nyuma "Televisheni ya Nyota na magazeti mengine yanayofanya kazi kwa ajili ya adui yalieneza habari za uongo" kuhusu jeshi.

Anaongeza kuwa kwa sababu ya hili, jeshi linaweza "kuchukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha kwamba nguvu ya sheria inaheshimiwa."

Radio Okapi ya ONU na vyombo vingine vya habari vinasema kuwa Televisheni ya Nyota inamilikiwa na mgombea urais Moïse Katumbi ambaye anafanya kazi katika jimbo la Katanga.

Televisheni ya Nyota inasema kwamba Baraza la Mawasiliano Conseil, ambalo linadhibiti shughuli za vyombo vya habari nchini DRC, imeondoa 'masafa' yake kutoka kwa laini ya kitaifa.

Frederic Kitengie, mkuu wa kituo cha Televisheni cha Nyota, alisoma taarifa iliyofichua hasira za wanajeshi dhidi ya kampuni na kwamba walimdanganya.

Televisheni ya Nyota inaripoti habari iliyochapishwa kwenye ukurasa mwingine wa Facebook uitwao Nyota Televisheni kwamba "nyumba ya mkuu wa jeshi [Jenerali Christian] Tshiwewe ilizingirwa, katika mpango ulioandaliwa na Jenerali Ntumba kukamata au kuondoa mamlaka ya juu kutoka Katanga".

Katika siku za hivi karibuni, vikosi vya DR Congo vimeongeza operesheni za usalama katika mji wa Lubumbashi katika jimbo la Katanga ambako mgombea urais Moïse Katumbi ana nguvu na aliwahi kuongoza.

Wakiwa nchini DR Congo kwa sasa wanahesabu kura na kusubiri matokeo ya uchaguzi, habari nyingi zimetawaliwa na uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kile kinachoendelea katika kipindi hiki cha kusubiri, hasa uvumi wa mapinduzi ya kijeshi.

Mkuu huyo wa kituo cha Televisheni cha Nyota alisema wanaotangaza hivyo si televisheni yao kwa sababu ni tofauti na walivyo 'dai' kwa namna inayoonekana kwenye 'nembo' na wafuasi wao kwenye mtandao wa Facebook.

Frederic Kitengie anasema kuwa FARDC ina uwezo wa kutosha “kuweza kuona kuwa hii si Televisheni ya Nyota halisi”, na anasema baada ya ukurasa mwingine wa Facebook waliweza kuwatambua watumiaji wake na kutokana na shinikizo wao wenyewe wakaifungia.

Wakati jeshi likisema huenda likachukua hatua, vyombo vya habari kama vile Televisheni ya Nyota vinalishutumu kwa "udhaifu na mgawanyiko", mashariki mwa nchi hiyo liko vitani na kundi la M23 kwa ushirikiano na vikundi vingine vinavyoitwa Wazalendo.

Wakati wa Krismasi, mapigano yaliripotiwa tena katika eneo la Masisi. Pande hizo mbili zilishutumu kila mmoja kwa kukiuka usitishaji vita wa wiki mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live