Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Kampeni Uchaguzi Mkuu kuhitimishwa leo

Tshisekedi Katumbi Urais.png DRC: Kampeni Uchaguzi Mkuu kuhitimishwa leo

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampeni za Uchaguzi Mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zinakamilika rasmi leo, Jumatatu Desemba 18.2023 wakati huu ambao Shirika la Kimataifa la kutetea Haki za Binadamu (Human Rights Watch) likitahadharisha kuwa ghasia zinazohusiana na uchaguzi zinatishia kuvuruga uchaguzi huo uliopangwa kufanyika mnamo siku ya Jumatano, Desemba 20.2023

Human Rights Watch imetoa wito kwa mamlaka za DRC kuchunguza haraka na bila upendeleo matukio ya vurugu yanayohusiana na uchaguzi na kuwashtaki waliohusika, bila ya kujali wanaegemea upande gani wa kisiasa

Mtafiti Mkuu wa Human Rights Watch Tawi la DRC Thomas Fessy ameeleza kuwa shirika hilo limeorodhesha matukio kadhaa ya vurugu yaliyotokea nchini humo ambapo inaonyesha wahusika ni miongoni mwa wafuasi wa vyama hasimu vya kisiasa ambavyo kiuhalisia vurugu zao zimesababisha mashambulizi ya kulipa kisasi, unyanyasaji wa kingono na kifo cha mtu mmoja hadi sasa

Aidha, inaelezwa kuwa zaidi ya watu milioni 1.5 hawataweza kushiriki zoezi la kupiga kura katika maeneo yenye mizozo, hasa katika jimbo la Kivu Kaskazini na jimbo la Magharibi la Mai-Ndombe

Pia mamilioni ya wakimbizi wa ndani pia huenda wasishiriki zoezi hilo,

Washindani wakuu wa Uchaguzi huo Rais Felix Tshisekedi anayeomba kutetea kiti chake na Rais wa Klabu ya Soka ya TP Mazembe Moise Katumbi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live