Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Jeshi limeripotiwa kushambulia ngome za M23 kwa kutumia ndege

DRC DRCCCCCC.png DRC: Jeshi limeripotiwa kushambulia ngome za M23 kwa kutumia ndege

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini DRC, jeshi la serikali limeripotiwa kufanya mashambulio kwa kutumia ndege, kulenga maeneo yaliodhibitiwa na waasia M23 siku ya Jumatano katika eneo la Kilolirwe na viunga vyake.

Kulingana na vyanzo katika eneo hilo, mashambulio ya FARDC yalilenga maeneo ya Kausa na Muyange katika eneo la Masisi, jimboni Kivu Kasakazini.Aidha vyanzo vimeripoti mapigano katika vijiji vya Rubona na Sisa, huku vingine vikiripoti hali ya ya utulivu kushuhudiwa hapo jana asubuhi katika maeneo ya Kibumba na Nyiragongo.

Katika hatua nyingine maelfu ya watu wameripotiwa kuendelea kukimbia makazi yao kufuatia kuzuka kwa mapigano mapya kati ya waasi wa M23 na makundi yenye silaha yanayounga mkono serikali.

Siku ya jumatano, watu walikimbia vijiji kadha huko Kilolirwe, huku mashirika ya kiraia, yakisema zaidi ya watu elfu 3 waliokimbia nyumba zao wanaripotiwa kuwasili mjini Sake.

Kulinganana Umoja wa mataifa, watu laki mbili zaidi wamekimbia nyumba zao tangu mapigano kuzuka tena mwezi uliopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live