Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Jeshi larejesha utulivu katika mji mdogo wa Sake uliodhibitiwa na M23

DRC: Jeshi Larejesha Utulivu Katika Mji Mdogo Wa Sake Uliodhibitiwa Na M23 DRC: Jeshi larejesha utulivu katika mji mdogo wa Sake uliodhibitiwa na M23

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa utulivu umerejea katika 'kituo' cha Sake huko Masisi baada ya maelfu ya watu kutoroka eneo hilo Jumatano na kukimbilia katika mji wa Goma.

Wizara ya Mawasiliano imetangaza kuwa serikali ilivipongeza vikosi vya FARDC kwa mashambulizi hayo, "ambayo yalifanywa kwa ujasiri na azma na kurejesha utulivu katika mji wa Sake".

Wakazi wengi wa mji huu mdogo uliopo kilomita 25 magharibi mwa Goma, wamekimbia tangu Jumatano iliyopita baada ya mapigano makali katika milima inayozunguka uzunguka Sake katika bonde linalopakana na Ziwa Kivu.

Siku ya Jumatano, kundi la M23 lilitangaza kwamba lilikuwa limeziteka kambi za jeshi la serikali kwenye milima ya Nturo 1, Nturo 2, na maeneo mengine yaliyopo karibu na Sake. Haijabainika iwapo vikosi vya serikali vimechukua tena milima hiyo.

Chanzo: Bbc