Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Hatuwezi kuzungumza na M23, hakuna nchi inayozungumza na 'magaidi'

DRC: Hatuwezi Kuzungumza Na M23, Hakuna Nchi Inayozungumza Na 'magaidi' DRC: Hatuwezi kuzungumza na M23, hakuna nchi inayozungumza na 'magaidi'

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Balozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa serikali ya nchi yake haiwezi kufanya mazungumzo na kikundi cha waasi wa M23, kwasababu hakuna nchi yoyote duniani ambayo imewahi kuzungumza na 'kikundi cha ugaidi’.

Balozi Georges Nzongola-Ntalaja ameyasema hayo katika kikao na B-araza kuu la usalama la Umoja wa Mataifakilichofanyika usiku wa Jumatano, kilichotaka kufahamu hali ya mambo katika eneo la maziwa makuu, hususan katika eneo la mashariki mwa DRC.

Katika hotuba yake, balozi wa Congo ameishutumu Rwanda kuwa chanzo cha matatizo ya kiusalama mashariki mwa Congo.

Akizungumza katika kikao hicho, Balozi wa Rwanda katika Umoja wa mataifa Claver Gatete pia aliishutumu DRC kuwa kikwazo cha mpango wa amani mashariki mwa nchi hiyo, kwa kukataa kufanya mazungumzo na kuwaunga mkono waasi wa kundi la FDLR wanaoipinga serikali ya Rwanda.

Balozi Gatete amesema “suala la M23 kukubali kujiondoa kwenye maeneo iliyokuwa imeyateka mashariki mwa DRC ambayo kwa sasa yamo mikononi mwa jeshi la kikanda”, inaonyesha kuwa M23 wako tayari kutekeleza makubaliano ya amani ya wakuu wa nchi yaliyofikiwa Luanda na Nairobi, akasema upande wa serikali ya Congo unafaa pia kutekeleza makubaliano hayo.

DRC imekuwa ikikabiliwa na mzozo ambapo jeshi la nchi hiyo, FARDC, linapambana na wapiganaji wa M23, ambao serikali inasema wanaungwa mkono na Rwanda. Rwanda imekuwa ikikanusha madai hayo.

Chanzo: Bbc