Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: CENI yatangaza matokeo ya Ubunge

Tume Ya Uchaguzi DRC Yafuta Uchaguzi Katika Majimbo Kadhaa DRC: CENI yatangaza matokeo ya Ubunge

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza matokeo ya awali ya wabunge yaliyokuwa yanasubiriwa, baada ya uchaguzi wa Desemba 20 mwaka uliopita.

Kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyotangaza Jumapili iliyopita na jana, na mwenyekiti wa CENI Dennis Kadima, tayari matokeo ya wagombea 688 yametangazwa kati ya waliokuwa wagombea zaidi ya 40,000 waliokuwa wanawania nafasi ya ubunge kote nchini.

Vyama mbalimbali vya siasa vinachuana vikali kudhibiti majimbo mbalimbali ya nchi hiyo kupitia uchaguzi huo, lakini inavyoonekana, matokeo hayo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa CENI Denis Kadima, chama cha UPDS chake rais Felix Tshisekedi na washirika wake wana idadi kubwa ya viti.

Kupitia muungano wa kisiasa wa Sacred Union, kinachoundwa na wanasiasa wengine kama Jean-Pierre Bemba, Vital Kamerhe na Modeste Bahati, wametabiriwa kuongoza katika majimbo mbalimbali ya nchi hiyo, likiwemo jiji kuu la Kinshasa ambalo ni ngome ya upizani.

Mbali na Kinshasa, jimbo lingine ambalo limeshuhudia ushindani mkali ni ngome ya mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi huko Katanga.

Hata hivyo, matokeo yaliyotangazwa, wagombea kutoka muungano wa rais Thisekedi, wameonekana kupata ushindi katika majimbo matano, hali ambayo inampa nafasi ya kuwa na wabunge wengi bungeni, huku upinzani ukiendelea kulalamikia matokeo hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live