Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Askari wawili wauawa mbugani

UGANDA DRC WAJEDA DRC:Askari wawili wauawa mbugani

Sun, 25 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askari wawili wa wanyama pori wameuawa na mwingine kujeruhiwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo katika Mbuga ya Kitaifa ya Virunga, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Eneo kubwa kwenye mpaka wa Uganda na Rwanda, Virunga ndiyo hifadhi kongwe zaidi barani Afrika na inajulikana ulimwenguni kote kama hifadhi ya wanyama adimu, wakiwemo sokwe wa milimani.

Lakini pia hutumika kama maficho ya vikundi vyenye silaha vinavyofanya kazi katika eneo hilo kwa miaka mingi.

Taasisi ya Uhifadhi wa Mazingira nchini Kongo (ICCN) ilmesema walinzi hao walikuwa wakishika doria katika eneo kuu la mbuga hiyo waliposhambuliwa na wanashuku washambuliaji hao ni wa kundi la "Mai-Mai"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live