Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Amuoa mwalimu wake ' Nilishindwa kusikiliza akifundisha'

DRC DRC AMUA MWALIMU (600 X 308) DRC: Amuoa mwalimu wake ' Nilishindwa kusikiliza akifundisha'

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja wa nchi ya DRC, Hassan Remy amemuoa aliyekuwa mwalimu wake wa sekondari na kusema alishindwa kumsikiliza alipokuwa akifundisha darasani.

Remy amesema alimchumbia Maombi Jeannette aliyemzidi miaka 12 baada ya kumaliza shule na baadaye kumuoa, licha ya uhusiano wao kupigwa vita na watu wengi.

Remy amesema anafurahia ndoa yake na mkewe, Maombi na sasa wamebarikiwa kupata watoto wawili.

Akifanya mahojiano na chaneli ya Afrimax English, baba huyo wa watoto wawili amesema alishindwa kuzingatia masomo wakati Maombi alipokuwa akifundisha.

"Nilikuwa najiuliza kama yeye na mimi tunaweza kuwa pamoja. Nilijua ningekabiliana na upinzani mkubwa, ikiwemo umri wake mkubwa kwangu," amesema Remy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live