DR Congo imesitishata shughuli za kampuni ya uchimbaji madini ya China katika Mkoa wa Tshopo kaskazini na kuwakamata wafanyakazi 16 huku kukiwa na mapitio ya shughuli za uchimbaji madini nchini humo.
"Xing Jiang Mining ilikuwa na leseni ya kufanya uchunguzi wake lakini haikuwa na kibali cha kuendesha shughuli za uchimbaji madini. (...) Lakini kwa bahati mbaya, tuligundua kuwa kampuni hii ilikuwa inaendesha shughuli za uchimbaji madini na ndiyo maana tukaiita uendeshaji shughuli haramu."
Waziri wa Madini wa Mkoa, Annelle Kamba. , alinukuliwa akisema na Radio Okapi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa.
Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi hivi karibuni alitoa wito wa kuangaliwa upya kwa mkataba wa uchimbaji madini na China.