Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DR Congo yaongeza muda utekelezaji sheria ya kijeshi

DR Congo Yaongeza Muda Utekelezaji Sheria Ya Kijeshi DR Congo yaongeza muda utekelezaji sheria ya kijeshi

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yaongeza muda wa sheria ya kijeshi kwa mara ya 45 katika mikoa ya mashariki ya Kivu Kaskazini na Ituri ambako uasi wa miongo kadhaa unaendelea.

Ongezeko hilo la siku 15 lilianza Jumapili, kulingana na Mishapi Voice Radio.

"Kulingana na Waziri wa Sheria Rose Mutombo, ambaye aliwasilisha mswada huo kwa Baraza la Seneti siku ya Jumamosi, lengo ni kuruhusu jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa na njia zote zinazohitajika ili kuendelea na operesheni za kijeshi na kukomesha kabisa ukosefu wa usalama unaoendelea katika eneo hili la mashariki mwa DR Congo,” redio hiyo iliripoti.

Hali ya kuzingirwa, ambayo ni utawala maalum wa sheria ya kijeshi, iliamuliwa katika majimbo hayo mawili na Rais Félix Tshisekedi mnamo Mei 2021.

Lengo lilikuwa kudhibiti ghasia za waasi waliotoroka katika majimbo hayo mawili kwa kuweka tawala za kijeshi na kuimarisha operesheni za usalama.

Uasi upya wa Vuguvugu la (M23) huko Kivu Kaskazini umeongeza shughuli zaidi huku rasilimali zikielekezwa kukabiliana na uvamizi huo.

Chanzo: Bbc