Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DR Congo yaitaka ICC kuchunguza madai ya uhalifu jimbo la Kivu

DR Congo Yaitaka ICC Kuchunguza Madai Ya Uhalifu Jimbo La Kivu.png DR Congo yaitaka ICC kuchunguza madai ya uhalifu jimbo la Kivu

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imemtaka mwendesha mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuchunguza uhalifu unaodaiwa kufanywa katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini humo tangu mwanzoni mwa mwaka jana.

Taarifa kutoka kwa mwendesha mashtaka, Karim Khan, inasema kuwa ofisi yake imeombwa "kuchunguza vikosi maalum vya kijeshi na vikundi" vinavyohusika na uhalifu unaodaiwa.

Hakuna majina maalum yaliyotajwa, lakini serikali ya DR-Congo imewahi kusema kwamba Rwanda ilikuwa inaunga mkono kundi la waasi la M23, ambalo limekuwa likishutumiwa kutekeleza ukatili.

Rwanda imekuwa ikikanusha tuhuma hizo.

Katika ripoti ya hivi majuzi, shirika la Human Rights Watch lenye makao yake mjini New York lilisema kuwa M23 "walitekeleza mauaji na kulazimishwa raia kujiunga nao", lakini wakaongeza kuwa jeshi la Congo "linashirikiana na na baadhi ya makundi ya wanamgambo".

Mzozo wa Kivu Kaskazini umesababisha maelfu ya wato kutoroka makwao.

Chanzo: Bbc