Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DR Congo yaishutumu Rwanda kwa ulaghai dhidi ya wakimbizi

DR Congo Yaishutumu Rwanda Kwa Ulaghai Dhidi Ya Wakimbizi.png DR Congo yaishutumu Rwanda kwa ulaghai dhidi ya wakimbizi

Thu, 12 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeilaani Rwanda kwa kusema haitawachukua tena wakimbizi wanaokimbia vita katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa upande wa Rwanda, Siku moja baada ya rais wa Rwanda Paul Kagame kutoa kauli tata kuhusu wakimbizi kutoka DRC kuingia Rwanda, Msemaji wa nchi hiyo amekanusha Rwanda kutoruhusu wakimbizi kuingia nchini humo.

Yolande Makolo amesema kuwa vyombo vya habari vimepotosha hotuba ya Kagame.

Msemaji wa serikali ya Congo amesema matamshi ya rais wa Rwanda Paul Kagame yanathibitisha kuwa haki za binadamu hazina thamani kwake. Aliishutumu Kigali kwa kuchafua jumuiya ya kimataifa kwa kutumia wakimbizi kwa madhumuni ya kisiasa.

Patrick Muyaya alisema ingawa Rais Kagame alijaribu kurejea maoni yake kuhusu suala hilo, "amefichua nia yake ya kweli". Zaidi ya Wakongo 70,000 wamevuka hadi Rwanda, wakikimbia mzozo kati ya serikali na waasi wa M23, ambao jumuiya ya kimataifa inasema inaungwa mkono na Rwanda.

Kigali inakanusha madai hayo. Mashariki mwa Kongo inakabiliwa na migogoro mingi, hasa kuhusu rasilimali za madini.

Chanzo: Bbc