Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DR Congo yaapa kuwaadhibu wanajeshi walio na uhusiano na kundi la waasi

DR Congo Yaapa Kuwaadhibu Wanajeshi Walio Na Uhusiano Na Kundi La Waasi DR Congo yaapa kuwaadhibu wanajeshi walio na uhusiano na kundi la waasi

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Jeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linasema kuwa litaadhibu askari yeyote atakayewasiliana na kundi kubwa la waasi wa Kihutu wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Jeshi lilisema yeyote - bila kujali cheo - ambaye alivunja marufuku ya kufanya shughuli zozote na wanamgambo wa FDLR atakamatwa.

Tangazo hilo linafuatia shinikizo kutoka kwa Marekani kwa Kongo na Rwanda kupunguza mvutano kati yao.

Rwanda inaaminika kwa kiasi kikubwa kuanzisha kundi la waasi la M23 linaloongozwa na Watutsi ili kukabiliana na FDLR - mamlaka ya Rwanda daima imekuwa ikikanusha madai ya kuunga mkono kundi hilo.

Chanzo: Bbc