Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DR Congo: Wanajeshi wa Rwanda walikamatwa na wanakijiji

Wanajeshi Rwanda Kukamtwa DR Congo: Wanajeshi wa Rwanda walikamatwa na wanakijiji

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa jeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anasema wanajeshi wawili wa Rwanda walikamatwa na wanakijiji, siku moja tu baada ya Rwanda kudai walitekwa na waasi wanaoiunga mkono serikali.

Wanajeshi hao wa Rwanda - Élysée Nkundabagenzi na Ntwari Gad - walikamatwa na wakazi wa eneo la kichifu la Bwisha, takriban kilomita 20 kutoka mpakani, kulingana na Jenerali Sylvain Ekenge.

Alidai kuwa wanajeshi hao wawili waliingia DR Congo Jumatano iliyopita kushambulia kambi ya kijeshi ya Runangabo kabla ya kukamatwa na wakaazi.

Siku ya Jumamosi Rwanda ilisema wanajeshi hao wawili walikuwa wakishikiliwa mateka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wanamgambo wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR, ambayo inasema inapata uungwaji mkono kutoka Kinshasa.

DR Congo imeongeza mashambulizi yake dhidi ya waasi wa M23 katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Waasi, ambao walikuwa wamefukuzwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 2013, wamejipanga upya na kuchukua maeneo ya kimkakati.

Rwanda imetuma wanajeshi katika mipaka yake na DR Congo kutokana na mapigano hayo.

Mkuu wa Umoja wa Afrika, Rais Macky Sall wa Senegal, ameeleza ‘’wasiwasi mkubwa’’ kutokana na kuongezeka kwa mvutano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live