Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DR Congo: Wakaazi wa Mushaki wameanza kurejea

Mushaki Wanavyorejea.png DR Congo: Wakaazi wa Mushaki wameanza kurejea

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakaazi wa mji wa Mushaki, umbali wa Kilomita 40 kutoka Goma Mashariki mwa DRC , sasa wameanza kurejelea shughuli zao za kawaida, baada ya kuondoka kwa waasi wa M 23 na eneo hilo kudhibitiwa na jeshi la FARDC kwa ushirikiano na lile la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nikiwa Kijijini MUSHAKE nimekutana Innocent Chirumwa amabye vita kati ya M23 vilisababisha kifo cha mke wake na watoto wake, hapa amethibisha kwamba amerejea kijijini mwake na kufanya kazi kama kawaida.

“Hapa maisha ni ya kawaida, tunafanya shughuli kama Kawaida, lakini hivi tuu majuzi kulikuwa na shida ya wana jeshi wazalendo wakati walikuwa wanaingia hapa mjini walikuwa wanazua wasiwasi ila kwa leo watu wanatulia” alisemaInnocent Chirumwa.

Chirumwa amethibitisha namna maisha yanavyoendelea kijijini Mushaki tangu kujiondoa kwa waasi M23 kijijini humo.

“Tunatembea bila shida, watu wanafanya kazi yao hali ambayo inaonyesha kwamba mambo yataendelea kuwa sawa.” aliongezea kusemaChirumwa.

Hata hivyo wakaazi kwenye kijiji hiki wamelitaka Jeshi la Congo kuzidisha jitihada za kuimarisha usalama wilayani Masisi.

“Tunachokiomba ni kuhakikisha usalama zaidi porini,ili tuupate uhuru pia wa kwenda mashambani.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live