Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DR Congo: Waasi wa M23 kukabidhi mji muhimu kwa vikosi vya Uganda

DR Congo: Waasi Wa M23 Kukabidhi Mji Muhimu Kwa Vikosi Vya Uganda DR Congo: Waasi wa M23 kukabidhi mji muhimu kwa vikosi vya Uganda

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Waasi wa M23 wanaondoka katika mji wa Bunagana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenda kwa wanajeshi wa kulinda amani wa Uganda, msemaji wa kundi hilo amesema.

Wanajeshi wa Uganda, wanaoaminika kuwa maelfu, walionekana wakivuka katika mji wa mpaka wa Bunagana siku ya Alhamisi mchana.

M23 inakabidhi mji huo Ijumaa asubuhi, msemaji wa waasi hao Meja Willy Ngoma aliambia BBC.

Waasi wanatekeleza makubaliano ya mikutano ya wakuu wa mikoa na wakuu wa majeshi huko Luanda, Bujumbura na Nairobi, Bw Ngoma anasema.

Bunagana ambayo waasi waliiteka Juni mwaka jana, iliwahi kuwa makao makuu ya kundi hilo ambalo linatakiwa kujiondoa katika maeneo yote ya Rutshuru, Masisi na Nyiragongo ambalo limekalia tangu mapigano yalipoanza tena mwaka jana.

Katika taarifa, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wamesema wanajeshi wao wanaenda Bunagana "kufanya kama jeshi lisiloegemea upande wowote huku Wakongo wakitumia muda kutatua matatizo yao ya kisiasa".

Burundi, Kenya tayari wamepeleka wanajeshi katika maeneo ambayo M23 wamekuwa wakiondoka, Sudan Kusini pia inatarajiwa kutuma wanajeshi.

Hali ya utulivu imetawala katika eneo lenye vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo zaidi ya watu laki tano wameyakimbia makazi yao.

Chanzo: Bbc