Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto na ODM Watoa Kauli Sawa, Huenda Kuna Kitu Kinapikwa

Defe5e3ea2d847d4 DP Ruto na ODM Watoa Kauli Sawa, Huenda Kuna Kitu Kinapikwa

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- DP Ruto alisema anaweza kufanya kazi na kinara wa ODM Raila Odinga kwa sababu tofauti zao ni za kisiasa

- Muda mfupi baadaye ODM ilitoa taarifa na kusema wataunda muungano na vigogo wanaodhaniwa kuwa mahasimu wao

- Taarifa hizo mbili zilionekana kama ishara ya urafiki unaoanza tena kati ya Baba na Ruto

Naibu Rais William Ruto Alhamisi Machi 25 alisema hana tofauti za kibinafsi na kinara wa ODM Raila Odinga.

Akiongea kwenye mahojiano na redio Citizen, Ruto alisema tofauti zao ni za kisiasa na wanaweza kufanya kazi pamoja ikibidi.

"Watu hufikiria niko na shida na Raila. Lakini si hivyo. Hizi tofauti ni za kisiasa tu. Kuna mambo ambayo huwa tunaskizana. Tumekubaliana kuhusu kuunda vyama vya kitaifa na anakabiliwa na matatizo kama yale napitia," alisema Ruto.

Mtangazaji Vincent Ateya alitaka kujua iwapo wawili hao wanaweza kuungana tena kwenye siasa za 2022.



"Kama mtu yeyote anataka kuungana nasikuendeleza vuguvugu la hustler, basi hatuna shida. Tutafanya kazi ppamoja," alisema DP.

Saa chache baada ya Ruto kusema hayo, chama cha ODM pia kilitoa taarifa kwa vyombo vya habari na kutangaza huenda kikaingia kwenye muungano na vigogo wanaodhaniwa kuwa mahasimu.

"Chama cha Orange Democratic Movement 'ODM kina panga muungano ambao utakuwa ni mkubwa na kutikisa nchi nzima huku ukiweka sura mpya ya siasa za Kenya kwa miaka ijayo," taarifa iliyotumwa na katibu wa ODM Edwin Sifuna ilisema.



Sifuna alisema chama cha ODM kinajulikana kwa siasa za kuwanufaisha walala hoi na kupigana na umaskini.

"Muungano wetu utakuwa ni wa wanasiasa wachanga ambao wana ajenda na sera kuhusu masuala ya kisasa. Tunajulikana kwa kuungana hata na mahasimu wetu. Hapo ndipo tunaelekea," taarifa hiyo iliongeza.

DP Ruto kwa sasa ndiye anaonekana kuwa hasimu mkuu wa kinara wa ODM Raila Odinga tangu wapeane talaka ya kisiasa 2007.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke