Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto na Familia Yake Wapokea Chanjo ya Masonko Kukabili Covid-19

Cce9e38faa7873df DP Ruto na Familia Yake Wapokea Chanjo ya Masonko Kukabili Covid-19

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto na familia yake Jumanne Machi 30 walipokea chanjo dhidi ya coronavirus.

Kulingana na ujumbe uliopakiwa kwenye ukurasa wa DP mtandaoni, Ruto na Mama Rachael walichanjwa wakiwa nyumbani kwao Karen.

DP alisema chanjo hiyo itasaidia katika kupigana na janga la coronavirus na kuwataka Wakenya kushiriki zoezi hilo.

"Chanjo ya COVID-19 ni salama na itasaidia katika kuokoa maisha na kukabili ugonjwa. Nawaomba Wakenya kushiriki zoezi hili ili tujilinde dhidi ya janga hili na maambukizi yake," alisema Jumanne.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke