Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto kuwafurusha wanasiasa wenye vurugu ndani ya UDA

Bf8b9f18fcaad63f DP Ruto kuwafurusha wanasiasa wenye vurugu ndani ya UDA

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto amewatahadharisha wanachama wa UDA ambao watazua vurugu wakati wa uteuzi wa chamaRuto amedai chama cha UDA ni cha demokrasia na kitafanya uteuzi wa haki na huru, hakuna mwanasiasa atakayebaguliwaAidha, Ruto amedai kwamba, wanachama watundu watafurushwa chamani iwapo hatafuata maagizo na sheriaNaibu Rais William Ruto ametishia kuwafurusha wanasiasa ambao watazua ghasia na vurugu wakati wa uteuzi katika chama chake cha UDA.

Akiwahutubia wagombea wa chama hicho kutoka eneo la Pwani, Jumanne, Oktoba 19, Ruto alisema yeyote atakayetumia nguvu au kusababisha mvutano chamani, atatimuliwa.

"Mgombea yeyote atakayetumia ghasia katika chama chetu hatakubaliwa, atafukuzwa mara moja, hapa UDA hatutaki vurugu,"Alisema DP Ruto.

Ruto pia aliwahakikishia wagombea wote wanaotaka kukitumia chama cha UDA kuwania nyadhifa mbali mbali kwamba kutakuwa na usawa katika kuwachagua wapeperushaji wa bendera.

Aidha, Ruto aliongezea kwamba hakuna tiketi itakayopeanwa kwa wagombea kinyume na matarajio ya wapiga kura.

Madai ya Ruto yanajiri siku chache baada ya kuibuka tetesi kwamba wandani wa karibu wa Naibu Rais watapewa kipaumbele katika uteuzi wa chama.

"Nikiwa kwenye mkutano wa mashauriano na wanachama 14 wa UDA kutoka eneo la Lamu, Kwale , Mombasa na Taita Taveta, niliwapa hakikisho kwamba chama cha UDA kitafanya uteuzi wa haki na huru, pia kitazingatia demokrasia,"Alisema Ruto.

Asilimia kubwa ya wanasiasa kutoka Mlima Kenya wamekihamia chama cha UDA wengi wao wakitokea chama cha Jubilee ambacho kinasemekana kusambaratika.

Ruto ametangaza kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao kupitia kwa chama hicho ambacho amekuwa akikipigia debe katika sehemu mbali mbali nchini.

Kigogo huyo anatarajiwa kumenyana na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ambaye ameidhinishwa na viongozi kadhaa baadhi yao kutoka eneo la Mlima Kenya kuwania urais kwa mara ya tano.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke