Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto awazawadi maimamu mbuzi wanne kusherehekea Idd

0c1d7063a8b9dc3c DP Ruto awazawadi maimamu mbuzi wanne kusherehekea Idd

Thu, 13 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Sehemu ya viongozi wa Kiislamu walimtembelea Naibu Rais William Ruto katika makazi yake ya Karen siku ya Jumatano, Mei 12

- Baraza la Maimamu Kenya na timu ya Ulamaa iliongozwa na Sheikh wa Msikiti wa Landhies, Sheikh Ahmed Athman

- Idd-ul-Fitr ambayo ni moja ya sherehe muhimu za Kiislamu huanza siku ya kwanza ya Shawwal

Naibu Rais William Ruto aliwaalika viongozi wa Kiislamu katika makazi yake ya Karen.

Viongozi hao chini ya mwavuli wa Baraza la Maimamu na timu ya Ulamaa waliongozwa na Sheikh wa Msikiti wa Landhies, Sheikh Ahmed Athman.

Wakati wa ziara yao, Ruto aliwazawadi mbuzi wanne kwa maandalizi ya sherehe za Idd-ul-Fitr Ijumaa, mei 14.

"Nilitoa mbuzi kwa maskini na Baraza la Maimamu Kenya na Ulamaa wakiongozwa na Sheikh wa Msikiti wa Landhies Ahmed Athman, miongoni mwa wengine kwa sherehe za Idd-ul-Fitr, Karen, kaunti ya Nairobi," Ruto alisema.

Ruto pia alitumia fursa hiyo kuwapongeza Waislamu kutimiza nguzo mojawapo ya dini hiyo ya kufunga kwa mwezi mmoja kuomba wakati wa Ramadan.

Serikali ilitangaza siku ya Ijumaa, Mei 14, 2021 kuwa siku ya mapumziko kote nchini wakati waumini wa dini ya kiislamu wakitarajiwa kusherehekea sikukuu ya Idd-Ul- Fitr.

Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i alitangaza kupitia kwa notisi ya gazeti rasmi la serikali Jumatano, Mei 5.

Sherehe hii huandaliwa kwa siku tatu na asubuhi ya siku ya kwanza, Waislamu hukusanyika kuomba.

Siku kuu nyingine muhimu kwenye kalenda ya Kiislamu ni Eid-ul-Adha, ambayo huadhimishwa baada ya kukamilishwa kwa Hija ya kila mwaka wakati wa Qurbani.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke