Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto asema ataendelea kutoa michango makanisani na kwa wasiojiweza

7987d35bf7ee24df DP Ruto asema ataendelea kutoa michango makanisani na kwa wasiojiweza

Mon, 12 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto amemjibu vikali Rais Uhuru Kenyatta baada ya madai aliyoyatoa Ijumaa, Julai 9 kwamba amekuwa akiwahonga vijana na pia kuwachochea Wakenya.

Akizungumza akiwa ibadani katika kanisa la Holy Ghost Christian Church mtaani Huruma siku ya Jumapili, Ruto alisema ataendelea kupeana michango yake ya kifedha kwa makanisani, vijana na kwa vikundi vya wanawake.

"Wakati ulikuwa ukitafuta kura ulikuwa ukipeana hata KSh 100 lakini hukuwahi sema ni hongo, mimi nikitoa michango kanisani, kwa wahudumu wa Boda boda na wamama wa kuuza mboga, inakuwa ni hongo kwa wananchi. Hatuwezi kuwa shupavu lakini sisi sio wapumbavu," Ruto alisema.

Ruto alitoa matamshi haya baada ya Rais kumkashifu kwa kuwachochea vijana badala ya kuleta maendeleo

" Raila akizungumza, huwa anatoa wazo au madai ya kuleta maendeleo au la kukuza miundo mbinu, anaelewa jinsi mambo yanavyostahili kufanywa, ningependa kusema pia Kalonzo huwa anazungumzia maendeleo tu sio kama wengine kazi yao ni kuzunguka nchi nzima wakiwahonga vijana na kuwachochea Wakenya," Alisema Uhuru akiwa ziarani Ukambani ambapo alikuwa ameandana na Raila na viongozi wengine.

Read also

Wacheni Kumuumiza Rais Uhuru Kichwa, Ruto Awambia Vinara wa Nasa

Uhuru alikagua miradi kadhaa Ukambani ikiwemo ule wa bwawa la Thwake kaunti ya Makueni linalokisiwa kugharimu zaidi ya KSh 85 bilioni.

" Ukiwahutubia Wakenya, jiepushe na matamshi ya uchochezi, kuwa na taratibu za kufanya kazi sio kurusha hongo kwa vijana bila kuwasaidia, Uhuru aliongezea.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke