Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto apuuza kikao cha Raila na wazito wa Mt Kenya

575474ad11fca5d6 DP Ruto apuuza kikao cha Raila na wazito wa Mt Kenya

Sat, 2 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto amepuuza hatua ya mabwanyenye wa Mt Kenya kumuunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga.

Raila alikutana na wazito hao wa Mt Kenya ambao wanaonekana kukubali kuwa 2022 ni wakati wake wa kuingia Ikulu.

Ruto alisema matajiri wa Mt Kenya Foundation walikutana na Raila ili alinde mali yao akiingia uongoziniAlitaka walala hoi pia kujipanga ili wainuke kiuchumi kupitia mfumo wake wa kisiasa wa bottom-up.

Akiongea Jumatano Septemba 29 wakati wa mazishi ya babake spika wa Nyeri John Kaguchia, Ruto alisema kundi la Mt Kenya Foundation linataka Raila alinde mali yao akiingia serikalini.

Hii ni baada ya kundi hilo kufanya kikao na Raila katika mkahawa wa Safari Park Septemba 28 ambapo alipata nafasi ya kuuza sera zake kuhusu Mt Kenya kwa wazito hao.

Ruto alisema kile kundi hilo linataka ni biashara zao kulindwa akisema walala hoi pia na wao wapewe nafasi ya kucheza kadi zao.

"Kenya hii kuna demokrasia, kama matajiri wanakutana ili serikali ilinde mali yao wengine pia waachwe wakutana wajue vile watajiinua kiuchumi. Sisi tunataka mfumo wa kuinua mama mboga na wengine wa pale chini ili pia na wao wapate mali," alisema Ruto.

Kwenye kikao hicho cha Jumanne, waliohudhuria walisema ilikuwa wazi kuwa wazito hao wameamua kuhakikisha Raila anaingia Ikulu 2022.

Kwa sasa Raila anaeonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kupata kura za Mt Kenya kutokana na urafiki wake na Rais Uhuru Kenyatta kupitia handisheki.

Alifanya ziara ya Mt Kenya hivi maajuzi na kupata mapokezi mazuri kiasi cha kuwapa wasiwasi wandani wa DP ambao wamekuwa wakipuuzilia uwezo wa Raila kuukwea Mlima.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke