Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto apokelewa kwa shangwe ngome ya ODM Raila Odinga

51fb0f0ac38cb656 DP Ruto apokelewa kwa shangwe ngome ya ODM Raila Odinga

Sat, 25 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais alizuru kaunti ya Migori Jumamosi kukutana na hustlers katika ngome ya hasimu wake Raila OdingaAlisema ana imani kuwa ataunda serikali ijayo kupitia chama chake kipya cha UDA na kuwataka wakazi kumuunga mkonoMamia ya wakaazi yalionekana yakimkaribisha DP kwa shangwe licha ya kuwa eneo hilo limekuwa ngome ya ODMNaibu Rais William Ruto Jumamosi Septemba 25 alipokelewa kwa shangwe katika ngome ya kisiasa ya kinara wa ODM Raila Odinga.

Ruto alitumia nafasi hiyo kujipigia debe akisema yeye ndiye suluhisho la amsaibu yanayowakumba walala hoi.

Ruto aliwarai wakazi kumuunga mkono akisema yeye wakati huu ameamua kuunda serikali ya hustlers.

Alikuwa pamoja na gavana wa kaunti ya Migoro Okoth Obado na video zilizochapishwa mtandaoni zilionyesha mamia ya wakazi yakimkaribisha DP kwa furaha.



Aliwashambulia kinara wa ODM Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta akisema kwa sasa wanaungana kumpiga kisiasa.

"Mimi mnajua 2007 nilisukuma kazi ya Baba mpaka akawa waziri mkuu, 2013 nilifanya ingine ya kusukuma Rais Uhuru mpaka akawa mshindi. Sasa wakati huu eti wanaungana kunipinga mimi," alisema Ruto.

"Raundi hii nimeamua nitasukuma kazi ya hustlers, ninataka nifanye kazi yetu. Na chama ya hustlers ni UDA," aliongeza Ruto.



Aidha DP aliahidi kuwa atawalinda Raila na Uhuru akishinda uchaguzi ujao na kuhakikisha maisha yao yako sawa.

"Mimi mnisaidie alafu hawa wadosi nitawachunga. Nitapatia hawa askari wengi kuwalinda," alisema Ruto.

Awali kulikuwa na wasiwasi kuhusu ziara hiyo ya Ruto baada ya ripoti kuibuka kuwa magenge ya vijana yalikuwa yamepangwa kumshambulia DP.

Aidha hatua ya Gavana Obado kumkaribisha DP kutasababisha mtafaruku kati yake na uongozi wa chama cha ODM.

Amekuwa akitajwa na wandani wa Raila kama mmoja wa mwiba ndani ya ODM akidaiwa kuwa muasi wa chama.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke