Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto apokelewa kwa shangwe West Pokot, sheria za Covid-19 zavunjwa

F990f34b10514619 DP Ruto apokelewa kwa shangwe West Pokot, sheria za Covid-19 zavunjwa

Sun, 20 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wakazi walijitokeza kumpokea naibu rais kwa shangwe na hakusita kuchukua nafasi hiyo kuendeleza sera zakeWakazi walisema wako tayari kujiunga naye kwenye chama chake kipya cha Wheelbarrow baada ya masaibu JubileeSheria za Covid-19 hata hivyo hazikufutwa huku wafuasi wake wakionekana bila maski licha ya kukongamana pakubwaNaibu Rais William Ruto Jumamosi Juni 19 alipokelewa kwa shangwe katika kaunti ya West Pokot alipokuwa kwenye ziara.

Wakazi wa eneo hilo walijitokeza kwa wingi kumpokea DP wakati wa ziara ya kuzinduliwa kwa chuo anuwai cha Kitelakapel Technical Training Institute.

Licha ya serikali kupinga mikutano yote ya kisiasa ili kukabiliana na maambukizi ya Covid-19, DP aliendelea na salamu zake kwa wakazi waliojitokeza kumpokea.

Sheria za Covid-19 hazikuzingatiwa huku wakazi wengi wakiwa bila maski na hata kukongamana kwa wingi.



Wanasiasa wamekuwa wakikashifiwa kwa kutozingatia sheria ambazo wizara ya Afya iliweka kama njia ya kukabiliana na janga hilo.

Kwa sasa, kaunti 13 zimeripoti kuongezeka kwa maambukizi ya coronavirus siku chache tu baada ya wanasiasa kuzuru Kisumu kwa sherehe za Madaraka Dei.

Wakati wa sherehe hizo, Rais Uhuru Kenyatta, Raila Odinga na DP Ruto walijumuika na wakazi ambao hawakuzingatia sheria za Covid-19.

Sasa serikali imelazimika kuweka kafyu ya kutokuwa nje kuanzia saa moja jioni hadi saa kumi asubuhi katika kaunti za Vihiga, Busia, Kisii, Nyamira, Kakamega, Kericho, Bomet, Bungoma, Trans-Nzoia, Kisumu, Homa-Bay, Siaya, na Migori.

Wizara ya afya ilisema asilimia ya maambukizi kwenye kaunti hizo ni 21 ikilinganishwa na maeneo mengine ambapo ni 9.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari za TUKO hapa

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke