Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto anatafuta usadizi wa Museveni kuingia Ikulu, Atwoli asema

846d570c2f2a4737 DP Ruto anatafuta usadizi wa Museveni kuingia Ikulu, Atwoli asema

Fri, 23 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Atwoli alisema ziara ya Ruto Uganda ni kutafuta mkono wa Rais Museveni katika azma yake ya kuingia Ikulu 2022Alidai kuwa DP yuko na njama ya kukataa matokeo ya uchaguzi huo ujao baada ya kurambishwa sakafuRuto amekuwa akisema amewashinda akili wapinzani wake na sasa wanachofanya ni kutapatapa kama mtu anayezamaKatibu wa muungano wa wafanyikazi nchini COTU Farncis Atwoli amesema anashuku ziara za Naibu Rais William Ruto nchini Uganda.

Ruto alikuwa nchini Uganda wiki mbili zilizopita ambapo alipokewa na Rais Yoweri Museveni katika kuweka msingi wa ujenzi wa jengo la Biological Drugs and mRNA katika eneo la Wakiso.

Atwoli anadai lengo la ziara hiyo ilikua kutafuta msaada wa Rais Museveni kwenye azma yake ya kuingia Ikulu.

Alisema huenda DP yuko na mpango wa kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu ujao na kwa sasa anajiandaa kuhusu hali hiyo.



Read also

Raila Hawezi Kubaliki Mt Kenya, Gavana Mutua Amwambia Rais Uhuru

Akiongea Tana River wakati wa ziara ya kinara wa ODM Raila Odinga, Atwoli alisema DP Ruto atabwagwa kinyang'anyiro cha 2022.

"Nataka nimwambie Raila Odinga kuwa Ruto atashindwa lakini hatakubali. Ndio ameanza kuungan na nchi jirani ili kujihami," alisema Atwoli.

Mwanaharakati huyo alisema Ruto ndiye wa kulaumiwa kutokana na kuharibika kwa uchumi humu nchini na kuonya kuwa akiingia Ikulu hali itakuwa mbaya zaidi.

Atwoli amekuwa mmoja wa wakosoaji wakuu wa DP Ruto wanaosema watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa hajaingia Ikulu kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.

Amekuwa akipendekeza mabadiliko ya kikatiba ili kubadili mfumo wa uongozi humu nchini kama njia moja ya kuhakikisha wapinzani wa DP wataungana na kuingia Ikulu.

hata hivyo, DP amekuwa akiwatania akisema yuko tayari kwa muungano wowote kutoka kwa wapinzani wake.

"Saa hii wanatapatapa tu, ukiona wanazunguka hivyo jua kimeumana," DP alisema kuhusu wapinzani wake.



Read also

Magazeti Jumatano, Julai 21: Kilonzo Adai Uhuru Anachezea NASA Shere

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke