Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto alimpigia Raila Simu Kumjulia Hali, John Mbadi asema

E57e21e914f6de1e DP Ruto alimpigia Raila Simu Kumjulia Hali, John Mbadi asema

Fri, 26 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Licha ya kuonekana kuwa mahasimu wakuu wa kisiasa DP Ruto na Raila wanaripotiwa huenda wakaungana kwa ajili ya 2022

- Mwenyekiti wa ODM John Mbadi hata hivyo anasema hajashuhudia mazungumzo yoyote ya kisiasa kati ya DP na Raila

- Alisema anachokijua ni simu ambayo DP alimpigia Raila alipokuwa mgonjwa kumjulia hali

Mwenyekiti wa ODM John Mbadi amekanusha kuwa chama cha ODM kiko kwenye mazungumzo ya muungano wa kisiasa na Naibu Rais William Ruto.

Mbadi alisema mazungumzo ambayo anajua kati ya DP na Raila yalikuwa ya kumjulia Baba hali yake baada ya kuugua Covid-19.

Akiongea kwenye mahojiano na runinga ya KTN, Mbadi alisema Ruto alimpigia simu Raila baada ya ripoti za kuugua Covid-19 akitaka kujua hali yake.

"Mazungumzo ambayo yamefanyika kati ya Raila na Ruto ni kupitia simu wakati naibu rais alikuwa akimjulia hali yake kiafya, hilo ninaweza kusema kwa uhakika," Mbadi alisema.



Kumekuwa na ripoti kuwa kuna karata ambayo inachezwa ya kuwaleta DP Ruto na Raila pamoja ili kuunda muungano wa kuingia Ikulu 2022.

Hayo yameibuka baada ya tofauti za kisiasa kuibuka kati ya DP na Rais Uhuru Kenyatta ndani ya chama chao cha Jubilee.

Licha ya awali Uhuru kutangaza kuwa atamuunga DP wake mkono kuongoza 'miaka yake kumi', mambo yamebadilika na sasa Ruto hajui mbele wala nyuma.



Kwenye mahojiano na redio Citizen, DP Ruto alisema siasa haina uadui na chochote kinawezekana.

Watu hufikiria niko na shida na Raila. Lakini si hivyo. Hizi tofauti ni za kisiasa tu. Kuna mambo ambayo huwa tunaskizana. Tumekubaliana kuhusu kuunda vyama vya kitaifa na anakabiliwa na matatizo kama yale napitia," alisema Ruto.

Chama cha ODM pia kilitoa taarifa na kusema kiko tayari kuunda muungano na wanaodhaniwa ni mahasimu wao wa kisiasa.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke