Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto alijaribu kumpigia simu Matiang'i baada ya kuzuiwa Airport

Fc7a5f3ca3458269 DP Ruto alijaribu kumpigia simu Matiang'i baada ya kuzuiwa Airport

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Baada ya kuambiwa hawezi kusafiri bila idhini DP Ruto alitoa simu na kumpigia Waziri Matiang'iWaziri huyo hata hivyo alikosa kujibu simu hiyo na kumlazimu DP kutafuta usaidizi wa mkuu wa utumishi wa ummaKutibuka kwa ziara ya DP kumezua nipe nikupe kati ya wandani wake na mahasimu wakeRipoti zaidi zinaendelea kuibuka kuhusu yaliyojiri katika uwanja wa ndege wa Wilson Jumatatu Julai 2 wakati safari ya Naibu Rais William Ruto kuenda Uganda ilitibuka.

Kulingana na wandani wa Ruto, DP alijaribu kupigia simu maafisa wakuu serikalini kujua ni kwa nini anazuiliwa kusafiri.

Kulingana na mwanablogu Dennis Itumbi ambaye hufanya kazi Karen kwa DP, Ruto alimpigia simu Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i.

Itumbi alisema Ruto alimpigia Matiang'i simu hiyo lakini waziri huyo alidinda kujibu na hivyo DP kulazimika kutafuta maelezo kwingineko.

Alisema alimpigia simu mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinyua ambaye alimwarifu DP kuwa hakukuwa na masharti yoyote ya kutafuta ruhusa ya kusafiri nje ya nchi.



Read also

Ruto 'Ang'olewa Kucha' na Habari Zingine Zilizotikisa Anga Wiki Hii

"Kutoka lini hilo linafanyika? Hatujatoa maagizo kama hayo, hufai kutafuta ruhusa kusafiri, ni nani anasema utafute idhini ya kusafiri?

"Kinyua alimuuliza DP baada ya kumpigia simu Fred Matiang'i ambaye alikataa kujibu simu yake," Itumbi alisema Kinyua alimwarifu DP.

Kutibuka kwa ziara ya DP kumezua hisia kali za kisiasa humu nchini huku wandani wake wakisema ilikuwa ni njama iliyopangwa na maafisa serikalini ili kumdhalilisha.

Katika mahojiano ya hapo awali, DP Ruto alisema kuwa hatua ya kumzuia kuondoka nchini ilichochewa na siasa kutokana na tofauto baina yake na bosi wake Rais Uhuru Kenyatta.

Akiongea Inooro FM Jumatano, Agosti 4, naibu rais alisema hatua ya kuzuia safari yake ilikusudiwa kumsukuma kuzozana na watu wengine serikalini.

"Nimekuwa naibu rais kwa miaka tisa na nimesafiri kwenda nchi nyingi kwa sababu za kikazi na za kibinafsi. Hamna siku hata moja nimetakiwa kumuomba yeyote ruhusa hadi hapo Jumatatu," Ruto alisema.

Read also

Magazeti ya Alhamisi, Agosti 5: Joyce Nyambura Azikwa Kando ya Mumewe

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke