Naibu Rais William Ruto amejitenga na madai ya kutowajibikia ahadi walizowaahidi Wakenya akiwa na Rais wakati wa kampeniRuto alidai kwamba amekuwa akipitia changamoto nyingi tangu uchaguzi mkuu wa 2017Kulingana na Ruto, alifanikiwa kufanya kazi kikamilifu muhula wa kwanza akiwa madaraniNaibu Rais William Ruto amekiri kwamba mambo yalianza kuzidi unga pindi tu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017.
Ruto aliiambia runinga ya Inooro Jumatano, Agosti 4, kwamba baada uchaguzi wa 2017 amekuwa akikumbana na changamoto nyingi zingine zilizopelekea yeye kupigwa teke na wandani wa Rais.
Aidha, Ruto amejitenga na madai ya kutowajibikia ahadi walizowaahidi wakenya akiwa na Rais wakati wa kampeni.
Ruto pia ameshikilia shaka maridhiano ya rais Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga machi 2018 almaarufu 'handshake'.
Read also
Matiang'i Sasa Ndiye DP, Ruto Alia Kuhusu Anayopitia Serikalini
"Labda uwe mgeni Kenya hii, niliambiwa nikae kando, na kulikuweko na waliokuja kumsaidia rais wakiwemo watu wa NASA waliokuja kusambaratisha mipango yetu ya chama (Jubilee party)" alisema Ruto.
"Naliweza kuwaajibikia Wakenya kwa miaka mitano ya kwanza kikamilifu kama naibu wa rais." Aliongeza Ruto.
Haya yanajiri siku chache baada ya seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen kudai kwamba Ruto ni naibu kikatiba lakini anayeendesha shughuli zake ni kinara wa ODM Raila Odinga.
Murkomen alikuwa akijibu kuhusu ni nani anayefaa kulaumiwa kwa kutotimiza ahadi za Jubilee.
"Unaweza mlaumu Ruto kwa mambo ambayo yametendeka miaka minne iliyopita? Yeye sio mmoja wa viongozi serikalini, yeye yupo kikatiba tu lakini naibu wa rais Kenyatta ni Raila Odinga." Alisema
Miezi michache iliyopita Ruto alikiri kwamba amehujumiwa kama naibu wa rais na hangependa mtu mwingine kuhujumika kwa njia hiyo.
"Nikipewa nafasi singependa kuona mtu mwingine akipitia yale napitia kama naibu wa rais." Ruto alisema katika runinga ya Inoor,"
Read also
Mpeni William Ruto Amani Baada ya Kumpokonya Majukumu Yake, Oscar Sudi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.