Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto ajitenga na UDA: "Mimi ni naibu kiongozi wa Jubilee"

5a7829df4ee49c5c DP Ruto ajitenga na UDA: "Mimi ni naibu kiongozi wa Jubilee"

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto amesisitiza kwa mara nyingine kuwa yeye sio mwanachama wa chama cha United Democratic Alliance (UDA).

Sheria ya Vyama vya Siasa 2022 inasema mwanasiasa anahitaji kujizulu kutoka chama alichomo kabla ya kujiunga na kingine, Ruto alidokeza kuwa atafanya kazi na wanasiasa wengine kutoka vyama vingine vya kisiasa kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Ruto alidokeza kuwa atashirikiana na wanasiasa wengine kutoka vyama vingine vya kisiasa kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2022 Hapo awali Naibu Rais alisema UDA ni gari atakalotumia katika safai yake ya kuelekea Ikulu 2022.

Akiongea akiwa huko Kinango Jumanne, Agosti 25, Ruto ambaye anamezea mate kiti cha urais alisema haelewi ni kwa nini mrengo mmoja wa Jubilee umekasirishwa naye.

"Mimi sio mwanachama wa UDA, mimi, William Ruto, ni naibu kiongozi wa chama cha Jubilee. Lakini tumeamua kuungana na wanasiasa na wabunge zaidi ya 150 wa vyama mbali mbali kufanya mazungumzo kuhusu taifa hili. Mimi ni mshiriki halisi wa Jubilee kama vile Dalu (Mbunge wa Kinango) yuko katika chama cha ODM, " aliwaambia waombolezaji.

Ruto alizungumza wakati wa hafla ya mazishi ya mamake Gavana wa Kwale Salim Mvurya mama Sada Mgalla Nyawa huko Kalalani, eneo bunge la Kinango, kaunti ya Kwale.

Sheria ya Vyama vya Siasa 2022 inasema mwanasiasa anahitaji kujizulu kutoka chama alichomo kabla ya kuhamia kingine, Ruto bado hajatangaza kung'atuka katika Jubilee.

Hata hivyo, mwanasiasa huyo mwenye busara amekuwa akionesha dalili kwamba siku za usoni atahamia chana cha UDA ambapo atagombea urais.

Wakati fulani mwezi Juni, alitangaza hadharani ushirika wake na UDA siku chache tu baada ya uongozi wa Chama cha Jubilee kutangaza kwamba mazungumzo yake ya muungano na Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) yalikuwa yakiendelea.

Naibu rais alisema UDA ni gari la mahasla ambalo litawahakikishia urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke