Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto afungiwa nje ya Ikulu wakati wa makaribisho ya Suluhu Kenya

746771ab31786a66 DP Ruto afungiwa nje ya Ikulu wakati wa makaribisho ya Suluhu Kenya

Wed, 5 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ruto Emmanuel Tallam alithibitisha DP hakualikwa katika Ikuluni kumpokea rais wa Tanzania Suluhu

- Tallam alisema Ruto alifuata kwenye televisheni akiwa afisini kwake Karen na kuongeza kuwa ni Ikulu pekee inaweza kueleza ni kwa nini hakualikwa

- Tofauti za Uhuru na Ruto zimekuwa zikidhihirika hadharanii huku rais akimshutumu naibu wake kwa kufanya kampeni za mapema akiwa angali afisini

Kuwasili kwa rais wa Tanzania Samia Suluhu nchini mapema mapema, Jumanne, Mei 4, kumefichua nyufa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Suluhu aliandaa safari yake ya kwanza Kenya Jumanne na alipokelewa Ikulu, Nairobi na Uhuru na maafisa wengine wa serikali, lakini Ruto hakuwepo kwenye hafla hiyo.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ruto Emmanuel Tallam alithibitisha naibu rais hakualikwa kwenye mkutano huo wa hadhi na kuongeza kuwa alifuatilia matukio kwenye runinga akiwa afisini yake ya Karen, The Standard liliripoti.

Tallam alisema DP pia alikuwa mitandaoni kwa shughuli zake binafsi ambapo aliwaalika viongozi kadhaa wa kanisa kutoka AIC Kajiado ambapo alimzawadi mmoja wa wachungaji, Daniel Lotuno gari la kifahari.

Mkurugenzi huyo wa mawasiliano alisema ni Ikulu pekee inaweza kueleza sababu ambazo naibu rais hakualikwa.

Kwamba Uhuru na naibu wake wanae;ekea njia tofauti sio siri tena na kwa muda, wawili hao pia wameacha kukana kwmaba nikweli uhasama upo.

Katika mahojiano na kituo kimoj cha runinga, DP alikiri kwamba Uhuru alimtaka achukue nafasi ya nyuma katika kuendesha shughuli za serikali ili aweze kuandaa urithi wake wakati anapojipanga kuondoka ofisini mnamo 2022.

"Katika kipindi cha pili, Rais aliamua kufanya mambo kwa njia tofauti, hilo naliheshimu .. mimi nimechukua nafasi ya nyuma kwa sababu tunataka kujenga urithi wa Rais Uhuru kwa sababu kwa muda mrefu tulikuwa na UhuRuto .. na watu wengine walijali na akasema labda inapaswa kuwa Uhuru kwa sababu ndiye Rais, "alisema mnamo Agosti 2020.

Kwa upande mwingine, Uhuru amekuwa akimtuhumu Ruto kwa kukaidi agizo lake la kujiepusha na siasa na kuzingatia utekelezaji wa Ajenda Kubwa Nne.

Mnamo Septemba 2020, Ruto pia alizua gumzo alipokosa kuhudhuria hafla muhimu katika Ukumbi wa KICC ambayo kilikuwa ya kutathmini hali ya COVID-19 nchini.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke