Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto: Tatizo la Kenya linaletwa na uongozi wala sio katiba

E1c4da6744ee966e DP Ruto: Tatizo la Kenya linaletwa na uongozi wala sio katiba

Wed, 19 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- William Ruto alisema viongozi wanapaswa kuzingatia masuala ambayo yanaathiri Wakenya moja kwa moja badala ya kuwagawanya

- Ruto alisema kurekebisha katiba hakutatatua matatizo ya Kenya kwa sababu tatizo kuu lipo katika uongozi

- Alikemea siasa za makabila na kusema kuwa jukumu la kuwaunganisha Wakenya ni la viongozi

Naibu Rais William Ruto amesema tatizo la taifa la Kenya liko katika uongozi wa nchi na sio katiba.

Naibu rais alisema hayo siku chache tu baada ya kusherehekea kubatilishwa kwa mchakato wa maridhiano (BBI) na Mahakama Kuu.

Akiongea katika makazi yake ya Karen ambapo alikuwa mwenyeji wa viongozi kadhaa kutoka Kajiado, naibu rais alisema viongozi wanapaswa kuzingatia masuala ambayo yanaathiri Wakenya moja kwa moja badala ya kuwagawanya.

"Ninataka kuwashawishi viongozi katika taifa letu kwamba kuna hali halisi katika nchi yetu kwa sisi sote kuungana na kuuweka kando ubinafsi," Ruto alisema.

Pia alizungumza dhidi ya siasa za ukabila na akasema viongozi wana jukumu la kuhakikisha nchi inasalia kuwa na umoja kama yeye na Rais Uhuru Kenyatta walivyokadiria wlipoingai uongozini.

Hisia zake zinajiri siku chache baada ya Mahakama Kuu kutangaza BBI ni kinyume cha katiba na kuitupilia mbali.

Baada ya uamuzi huo Ruto alichapisha ujumbe kwenye kurasa zake mitandaoni akishukuru Mungu kwa uamuzi wa jopo la majaji watano.

Hatua hiyo haikupokelewa vyema na wabunge wa Kieleweke ambao walimsuta kwa kukataa kumuunga mkono miradi ya rais Uhuru.

"Tunasikitishwa sana na hatua ya naibu rais. Baada ya mahakama kuu kutupilia mbali BBI alianza kumshukuru Mungu kuhusiana na uamuzi huo, lazima suala hilo tutalirejelea baadaye," Mbunge Ngunjiri Wambugu alisema.

Wambugu pia alisema kwamba ingawa Ruto wakati wote alikuwa amebuni msimamo wa kutounga mkono BBI, hatua yake ya kusherehekea uamuzi wa majaji ilidhihirisha ni kweli alikuwa akipinga vikali mchakato huo.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke