Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto Avuna Jubilee, Wamuchomba na Gikaria Wajiunga na Tangatanga

15a6abba9d4e9bc4 DP Ruto Avuna Jubilee, Wamuchomba na Gikaria Wajiunga na Tangatanga

Wed, 23 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wamuchomba Jumatano aliamua kujiunga na kambi ya kisiasa ya DP Ruto baada ya kipindi ndani ya nyumba ya KielewekeWamuchomba alisema amefuata sauti ya wafuasi wake ambao wanataka ahubiri injili ya Ruto kwenye safari ya kuingia Ikulu 2022Hatua ya mwanasiasa huyo imezua mdahalo mitandaoni kwani alikuwa mkosoaji sugu wa DPNaibu Rais William Ruto Jumatano Juni 23 alipokea wafuasi wapya kwenye hema yake ya Tangatanga ambayo imeweka wazi kuwa inaingia chama cha UDA.

Ruto aliwapokea mwakilishi wa kina mama kaunti ya Kiambu Gathoni Wamuchomba na mbunge wa Nakuru Mjini David Gikaria.

Wawili hao wamekuwa ndani ya mrengo wa Rais Uhuru Kenyatta wa handisheki ambapo wamekuwa wakimkosoa DP vikali.

Kwenye safari hiyo ya kubatizwa kutoka Kieleweke na kuingia kikosi cha Tangatanga, wanasiasa hao waliongozwa na Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri.

Wabunge Samuel Gachobe wa Subukia na Kago wa Lydia pia waliungana na wenzao kuingia Karen ambapo DP amekuwa akicheza siasa zake kwa upole.

Wamuchomba alianza kubadili mkondo wa siasa zake baada ya matokeo ya uchaguzi wa Juja ambapo mgombea wa Jubilee Susan Wakapee alibwagwa na ule wa PEP.

"Huku Nyuma ya hema" kumejaa; hakuna viti, sijui kama Mheshimiwa Soipan atanipea kiti ama nijipange.........naskia wengine wanakalia hurubarrow. Na kwanza simu yangu imezima moto nafikiria niko na missed koll nyingi kuanzia Jumamosi . . . yule wa team kimeumana; prisi waambie wasinipigie bado nashauriana huku 'nyuma ya hema," alisema wakati huo.



Gikaria alikuwa mmoja wa wabunge wa Kieleweke ambao walipigia debe mgombea wa Jubilee wakati wa uchaguzi mdogo wa London Nakuru.

Amekuwa akiungana na mwenzake wa Nakuru Magharibi Samuel Arama kutetea Rais Uhuru Kenyatta na Jubilee katika kaunti ya Nakuru.

Hatua ya wao kuingia Tangatanga itakuwa pigo kubwa kwa kambi hiyo kwenye safari ya kuingia Ikulu 2022.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke