Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DP Ruto Afanya maombi afisini baada ya kumfinya Rais Uhuru Kiambaa

21cdbe4777b02bea DP Ruto Afanya maombi afisini baada ya kumfinya Rais Uhuru Kiambaa

Fri, 16 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ruto alionekana afisini akifuatilia maombi yaliyokuwa yakifanywa na Njuguna baada ya kutangaza mshindiKijana huyo wa UDA aliibuka mshindi kwa kujizolea kura 21773 dhidi ya mpinzani wake Kariri Njama aliyepata kura 21263Chaguzi hizo ndogo zilionekana kama maandalizi ya hali itakayokuwa kwenye uchaguzi mkuu ujaoVideo ya Naibu Rais William Ruto akifanya maombi afisini baada ya mgombea wa chama chake cha UDA kuibuka mshindi Kiambaa imeibuka.

DP Ruto anaonekana afisini akiwa pamoja na Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi wakifuatilia kutolewa kwa matokeo hayo.

Baada ya Tume huru ya mipaka na uchaguzi IEBC kumtangaza Njuguna Wanjiku cheti cha ushindi, aliamua kumshukuru Mungu.

DP anaonekana akifuatilia maombi yaliyofanywa na mgombea huyo mchanga aliyeishinda serikali.

"Tulipokuwa tukifanya kampeni tulisema tukipata ushindi tutamshukuru Mungu, na ndio nataka tushukuru Mungu kwa sababu mambo yamekuwa magumu lakini ametusaidia," alisema Njuguna.

Read also

Magazeti Ijumaa: Babu wa Miaka 93 Afunga Ndoa na Kipusa wa Miaka19

"Tuombeeni,Mungu ibariki Kiambaa, Mungu ibariki Kenya!" Wanjiku alisema huku DP Ruto akifuatilia maombi hayo kupitia afisini mwake ambapo pia alifanya ombi lake.

Njuguna aliibuka mshindi kwa kujizolea kura 21773 huku mpinzani wake Kariri Njama wa Jubilee akipata kura 21263.

Uchaguzi huo ulikuwa na umuhimu mkubwa kwa DP Ruto katika vita vya kisiasa dhidi yake na wandani wa Rais Uhuru Kenyatta kwenye Jubilee.

Njuguna alimshukuru DP kwa msaada aliompa wakati wa kampeni hizo akisema ulichangia ushindi wake.

"Nataka nishukuru DP Ruto kwa kuwa na imani na Hustler Nation na kwa msaada wake," alisema mbunge huyo mteule.

Katika wadi ya Muguga kaunti hiyo ya Kiambu, Jubilee ilipata ushindi baada ya mgombea wake kushinda kwa kura 27.

Chaguzi hizo ndogo zilionekana kama maandalizi ya hali itakayokuwa kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Read also

Mwakilishi wa Wanawake Laikipia Cate Waruguru Adokeza Kukihama Chama cha Jubilee

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke