Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DNA yathibitisha mjukuu wa Moi ndiye baba mzazi wa watoto aliowakataa

942fa220172902c6 DNA yathibitisha mjukuu wa Rais Moi ndiye baba mzazi wa watoto aliowakataa

Thu, 26 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Uchunguzi wa DNA uliofanywa katika maabara Hospitali ya Lancet mjini Nakuru umeonesha kuwa Collins Kibet Moi ndiye baba wa watoto hao kwa 99%. Kibet alishtakiwa na mke wake wa zamani Glady Jeruto Tagi mnamo Aprili 2021, kwa kukataa kuwatunza wanae.

Jeruto anataka Kibet awe akitoa KSh1 milioni kila mwezi kugharamia malezi ya watoto waoUchunguzi wa chembechembe za vinasaba (DNA) umethibtisha kuwa mjukuu wa marehemu Daniel Moi, Collins Kibet Moi ndiye baba halisi wa watoto wawili anaodaiwa kuwatelekeza

Matokeo hayo yaliwasilishwa katika Mahakama ya Nakuru, Jumatano, Agosti 25, wiki tatu baada ya Kibet kukubali kutii agizo la mahakama la kumtaka afanyiwe uchunguzi wa DNA kuthibitisha ikiwa yeye ndiye baba mzazi wa watoto hao.

Ripoti hiyo ya uchunguzi wa DNA uliofanywa katika maabara Hospitali ya Lancet mjini Nakuru mnamo Julai 2021, ilionyesha kuwa Kibet ndiye baba wa watoto hao kwa 99%.

Kibet alishtakiwa na mke wake wa zamani Glady Jeruto Tagi mnamo Aprili 2021, kwa kukataa kuwatunza wanao.

Hata hivyo, ajabu ni kwamba Kibet alipinga na kutaka uchunguzi wa DNA ufanywe ili kudhihirisha iwapo ndiye baba mzazi wa watoto hao wenye umri wa miaka tisa na 11.

Jeruto aitisha KSh1 milioni ya maleziKatika kesi aliyowasilisha Jeruto, anataka Kibet awe akitoa KSh1 milioni kila mwezi kugharamia malezi ya watoto wao.

Jeruto alidai kuwa Kibet alikimbia wajibu wake wa kugharamia malezi ya watoto hao kwa miaka minane.

Adharau MahakamaMnamo Julai 14,2021, Kibet ambaye ni mtoto wa marehemu Jonathan Toroitich alisukumwa gerezani kwa kosa la kudharau amri za mahakama.

Kibet alikwepa kuhudhuria vikao vya mahakama na pia kususia kujiwasilisha kufanyiwa uchunguzi wa DNA.

Hakimu Mkuu Benjamin Limo aliamuru kukamatwa kwake hata hivyo, baadaye alimwachilia huru kwa dhamana ya KSh100,000.

Hii ni baada ya kujitetea akisema akiiomba mahakama radhi akidai kuwa kuwa kutofika kwake hospitalini kulichangiwa na kukatika kwa mawasiliano kati yake na mawakili wake.

Askofu akiri kuzaa na muumini wa kanisa lake

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke