Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coronavirus: Kenya yarekodi visa vingine 646

COVID Coronavirus: Kenya yarekodi visa vingine 646

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Idadi ya maambukizi ya COVID-19 iliongezeka hadi 181,885 baada ya watu wengine 646 kuambukizwa virusi hivyo hatari kutokana na ripoti mpya ya Wizara ya Afya.

Wizara huyo mnamo Ijumaa, Juni 25 ilitangaza kuwa idadi hiyo ilithibitishwa baada ya sampuli 6,429 kupimwa katika saa 24 zilipoita.

Takwimu kutoka Wizara hiyo aidha zimefichua kuwa jumla ya sampuli zilizopimwa tangu Mwezi Machi kisa cha kwanza cha coronavirus kilipotia nchini zimefika 1,933,402.

"Kati ya visa vipya vilvyorekodiwa Wakenya ni 626 nao raia wa kigeni ni 20. 351 ni wanaume na wanawake ni 295. Mgonjwa mwenye umri wa chini ni mtoto wa miezi saba naye mkongwe zaidi ana miaka 92," taarifa ya Wizara ya Afya ilisema.

Kaunti ya Nairobi ilirekodi maambukizi ya juu zaidi na visa 115, huku Siaya ikifuata kwa visa 83 na Kisumu 67.

Aidha wagonjwa 1,017 wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini nao 6,653 wanahudumiwa wakiwa manyumbani mwao.

Wagonjwa wengie 102 nao wamelazwa wakiwa hali mahututi.

Idadi ya waliopata nafuu nchini imetimia 123,853 baada ya wagonjwa wengine 391 kuripotiwa kupona. Wagonjwa 211 wlaikuwa wakipokea matibabu nyumbani nao 180 walikuwa wakihudumiwa katika hospitali mbali mbali.

Wakati uo huo, idadi ya vifo vilivyosababishwa na COVID-19 imefikia 3,556 baada ya wagonjwa 18 kufariki dunia.

Maambukizi yalirekodiwa kamaifuatavyo; Mombasa 55, Busia 46, Uasin Gishu 34, Nakuru 32, Kakamega 31, Kisii 29, Vihiga 17, Kericho 16, Kiambu 16, Meru 14, Machakos 14, Homa Bay 13, Nandi 8, Bungoma 7, Trans Nzoia 7, Kilifi 7.

Kajiado 6, Turkana 4, Murang’a 3, Kwale 3, Nyeri 3, Garissa 2, Laikipia 2, Narok 2, Nyandarua 2, Kitui 2, Wajir 1, West Pokot 1, Baringo 1, Elgeyo Marakwet 1, Marsabit 1 na Migori 1.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke