Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Corona yapandisha gharama za usafirishaji

30cd7417073f5eaba59ef4f921a6817c Corona yapandisha gharama za usafirishaji

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WASAFIRISHAJI wa bidhaa za mboga, matunda na maua, wameomba kupunguzwa gharama za usafi rishaji zilizoongezeka kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa covid-19 ili kurahisisha ufanyaji biashara hiyo.

Wasafirishaji hao wamedai kuwa, kabla ya mlipuko wa ugonjwa huo, mashirika ya ndege ya kusafirisha mizigo, Shirika la Ndege la RwandAir lilikuwa likitoza dola za Marekani 1.2 kwa kilo moja lakini sasa walitoza dola 1.8 kwa kilo, huku Shirika la Ndege la Ethiopia awali lilikuwa likitoza dola za Marekani 1.4 kulingana na kiwango kinachosafirishwa, lakini kwa sasa kilo moja inasafirishwa kwa dola 2.2.

Mkurugenzi wa kampuni ya Almond Green Farm Ltd, Robert Rukundo, inayoshughulika na usafirishaji wa bidhaa hizo nje ya nchini, alisema kupanda kwa gharama hizo kumesababisha athari kubwa katika biashara zao.

Alisema pamoja na kupanda gharama za usafirishaji, lakini pia kwa sasa soko ni dogo. Alisema hali imeathiri ufanyaji biashara kwani yeye binafsi mauzo yake yamepungua kutoka tani 3-5 mpaka kati ya tani 1.2 mpaka 1.5 kwa wiki.

Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa NAEB, Pie Ntwari, alisema wanafahamu suala hilo na wanafanya mikakati ya kupata ufumbuzi.

“Tumekuwa na mikutano na RwandAir Ltd pamoja na Ethiopian Airways ambayo yanatoa huduma za usafirishaji nje ya nchi, pia tumefanikiwa kutoa ruzuku kwa viwango vya tozo za usafiri zilizoongezeka tangu kulipuka kwa ugonjwa huo,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz