Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Corona yaitega Stars Chan

98293 Pic+stars Corona yaitega Stars Chan

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

HATIMA ya kufanyika kwa mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) mwaka huu huko Cameroon kutokana na mlipuko wa homa kali ya mafua ijulikanayo kwa jina la Corona itajulikana baadaye. Ugonjwa huo ambao umekuwa ukisambaa kwa kasi duniani ukianzia China, unatajwa kuingia Cameroon ambako ndiko Fainali za Mashindano hayo zitafanyika mwaka huu kuanzia Aprili 4 hadi 25 huku timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ikiwa ni miongoni mwa timu 16 zitakazoshiriki mashindano hayo ikiwa imepangwa kundi D sambamba na Zambia, Namibia na Guinea. Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetoa taarifa ya kufuatilia kwa ukaribu kusambaa kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa huo na limeahidi kuchukua hatua stahiki mara baada ya uchunguzi wake kukamilika ili kuchukua hatua ya kufanya kwa mashindano yake, ikianzia Chan ambayo itafanyika mwezi ujao. “Caf inafuatilia kwa ukaribu kugundulika kwa hali ya ugonjwa huo wa mlipuko unaoathiri Bara letu. Nchi nane zimeripotiwa kuwa na waathirika ambazo ni Misri, Algeria, Tunisia, Morocco, Nigeria, Senegal, Cameroon na Afrika Kusini. "Timu imeundwa chini ya usimamizi wa Rais wa Caf ikiwa na wataalam wa masuala mbalimbali hasa ikijumuisha wa tiba hasa wale wanaojikita na afya za wachezaji  na wanachama wa familia ya mpira wa miguu Afrika,” limefafanua tamko la Caf lililotolewa jana. Taarifa hiyo imesema kuwa tume hiyo kwa kiasi kikubwa itajikita katika nchi ambazo zimepewa fursa ya kuandaa mashindano mbalimbali ya soka Afrika yanayosimamiwa na Caf.

Chanzo: mwananchi.co.tz