Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Corona kuahirisha nusu fainali Afrika

3fe779383cb630220a516c7f4c08890e Corona kuahirisha nusu fainali Afrika

Fri, 30 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MCHEZO wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika kati ya Raja Casablanca na Zamalek uliopangwa kufanyika Jumapili jijini Cairo, Misri uko katika hatihati ya kufanyika baada ya baadhi ya wachezaji wa mabingwa hao wa Morocco kukutwa na virusi vya corona.

Wiki iliyopita, Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) liliahirisha mchezo wa pili wa hatua hiyo ya nusu fainali baada ya wachezaji nane wa Raja kukutwa na virusi vya corona.

Baada ya vipimo vingine kufanyika Jumanne kesi mpya za corona sasa zimefikia 14 baada ya wachezaji wengine kupatikana na virusi hivyo.

Wachezaji sita wa Raja walitarajia kupimwa tena, huku wa kikosi chote walitakiwa kupimwa jana Alhamisi.

Kiongozi wa Mawasiliano wa Caf alisema mazungumzo yanaendelea na mamlaka za Misri kuhusu mchezo huo wa nusu fainali na fainali (Novemba 6) kwa sababu ya uchaguzi wa wabunge nchini Misri.

"Tunajadiliana nao kuhusu njia nzuri ya kufanya,” alisema Alex Siewe.

Caf imeruhusu Raja kuongeza wachezaji watatu kutoka katika kikosi chao cha timu ya vijana kujiunga na msafara wa timu hiyo ambao unatarajiwa kundoka leo Ijumaa kwenda Misri.

Mabingwa hao wa Morocco walipoteza 1-0 kwa Zamalek katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini hapa mapema mwezi huu na inapambana ili kuhakikisha inaifunga timu nyingine ya Misri, Al Ahly, katika fainali ya mwezi ujao.

Chanzo: habarileo.co.tz