Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Corona inaua zaidi wanaume kuliko wanawake Afrika

Screenshot 2021 03 05 At 22.19.11 660x400.png Corona inaua zaidi wanaume kuliko wanawake Afrika

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Umoja wa Mataifa umesema leo kuwa virusi vya corona vinasababisha vifo kwa wanaume wengi zaidi barani Afrika kuliko wanawake ambao kwa sehemu kubwa waandamwa na uwezekano wa kupoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi kuliko Covid-19.

Utafiti uliofanywa kwenye nchini 28 za Afrika, ikiwemo Guinea, Mauritius na Uganda umeonesha kwa wastani idadi ya wanawake waliopata maambukizi au kufa kwa corona ni ndogo ikilinganishwa na wanaume.

Takwimu zilizokusanywa zinaonesha kwa wastani asilimia 41 ya wanawake barani Afrika ndiyo wamekumbwa na janga la corona lakini idadi hiyo inatofautiana miongoni mwa mataifa.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kanda ya Afrika Matshidiso Moeti amesema kwa wanawake janga la covid-19 limesababisha ukosefu wa huduma za uzazi na wengi wanaweza kufariki kwa sababu hiyo kuliko matatizo yanayotokana na virusi vya corona.

MDOGO WA MMILIKI WA LA CHAAZ ASIMULIA BAR ILIVYOUNGUA “TUMEPATA HASARA KUBWA, HATUJAOKOA KITU”

Chanzo: millardayo.com