Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Corona: Wazikaji wagoma Afrika Kusini, vifo vyaongezeka

Uluhyoxqdmrufsrgxcr5f15cb354043b 660x400 Corona: Wazikaji wagoma Afrika Kusini, vifo vyaongezeka

Wed, 16 Sep 2020 Chanzo: millardayo.com

Moja ya kuifahamu leo September 16, 2020 ni hii ya takribani wazikaji 3,000 wameandamana nchini Afrika Kusini wakitaka kulipwa vizuri pamoja na mazingira mazuri ya kufanya kazi yao.

Wazikaji hao wamegoma kuchukua miili ya watu waliofariki majumbani mwao, hospitali pamoja na kuendesha shughuli za uzikaji wa miili hiyo.

Waandamanaji hao wanaishinikiza serikali kuanzisha mfuko wa virusi vya corona ambao utawapa nafuu kwenye ufanyaji kazi zao.

Gharama ha uzikaji au uchomaji moto wa miili ya watu waliofariki imeongezeka  kwa hadi 25% tangu kuanza kwa janga la corona nchini Afrika Kusini. Ongezeko hilo limechangiwa na uhitaji wa mavazi ya kujikinga (PPE), vipukusi (sanitisers) na vifaa kinga vinginevyo. 

Mamlaka zimesema kuwa kuna hatari ya mgomo huo ukahatarisha usalama wa afya za watu.

WANNE WALIONUSURIKA AJALI YA MOTO WAPELEKWA BUGANDO “ZIMAMOTO WAONGEA”

Chanzo: millardayo.com