Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Congo yakanusha kufanya shughuli za kijeshi na Uganda

CONGO VIOLENCE2 Congo yakanusha kufanya shughuli za kijeshi na Uganda

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekanusha kuwa imekubali kufanya operesheni za pamoja na jeshi la Uganda kuwawinda waasi wanaotuhumiwa kufanya mashambulizi ya mabomu ya kujitoa muhanga mjini Kampala, ikisisitiza kuwa nchi hizo mbili zinabadilishana tu taarifa za intelijensia.

Ripoti za kuwepo kwa kampeni hiyo ya pande zote za mpakani, ambazo zilithibitishwa na vyanzo viwili vya kidiplomasia, zimezusha wasiwasi miongoni mwa baadhi ya Wakongo, wanaokumbuka jukumu la Uganda katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomazilika mwaka wa 2003.

Msemaji wa serikali ya Congo Patrick Muyaya amesema majeshi ya nchi hizo mbili yamekuwa yakibadilishana habari kwa miezi mingi, na kuwa hakuna wanajeshi wa Uganda walioko nchini Congo kwa sasa.

Amesema kile serikali ilisema ni kuwa kutakuwa hatua za pamoja za kupambana na waasi na wala sio operesheni za pamoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live