Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Congo yaishutumu Rwanda kufadhili waasi

Congo Congo Congo yaishutumu Rwanda kufadhili waasi

Tue, 29 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linasema kuwa wanajeshi wa Rwanda waliwasaidia waasi wa M23 wakati wa shambulio la Jumatatu karibu na mpaka wake na Rwanda na Uganda.

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limesema limewakamata wanajeshi wawili wa Rwanda waliohusika na shambulizi hilo na kuwawasilisha katika mkutano na waandishi wa habari.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa msemaji wa serikali ya Rwanda, msemaji wa jeshi na mwanasheria mkuu hawakujibu maombi ya kutoa maoni yao.

Katika taarifa, jeshi la Congo limesema waasi walishambulia maeneo yao huko Tshanzu na Runyonyi.

Ilisema "hatua zote zimechukuliwa ili kurejesha mamlaka haraka" katika mikoa hiyo miwili.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukishutumu Rwanda na Uganda kwa kuunga mkono M23 ingawa serikali zote mbili zinakanusha madai hayo.

Kundi hilo la waasi, linaloundwa na waasi wa jeshi ambao wengi wao ni wa kabila la watutsi, lilipewa jina baada ya mkataba wa amani wa Machi 23, 2009 uliotiwa saini na serikali na wanamgambo wa zamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live