Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Congo: Serikali yawataka raia kujiepusha na matamshi ya chuki na unyanyapaa

Mgogoro Congooo Serikali yawataka raia kujiepusha na matamshi ya chuki na unyanyapaa

Wed, 22 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewataka watu kuepuka matamshi ya chuki na unyanyapaa. Katika siku chache zilizopita, ujumbe wa kuhimiza ghasia dhidi ya raia wa Rwanda zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini sauti zaidi zinawahukumu. Haya yanajiri huku kukiwa na mvutano kati ya DRC na Rwanda. Congo inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, tuhuma ambayo Kigali inakanusha.

Msemaji wa serikali ya Congo Patrick Muyaya ameahidi kwamba wale wote wanaotishia kuwashambulia Watutsi watakamatwa na watakabiliwa na mkono wa sheria.

Miongoni mwa watu waliozungumza dhidi ya vitendo hivyo, ni mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel,ni daktari maarufu Denis Mukwege.

Wiki chache zilizopita, alitoa wito kwa watu kutotumbukia katika hotuba za kibaguzi ambazo kulingana naye, zitawanufaisha tu maadui wa DRC.

Kuhusu mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, alikumbuka kuwa unyanyapaa wa sehemu ya jamii unadhoofisha mshikamano wa kitaifa, ambao ni muhimu katika nyakati kama hizi za mgogoro.

Alitoa wito kwa serikali ya Congo kuwafungulia mashtaka waandishi wa ujumbe unaochochea uhasama dhidi ya watu kulingana na makabila yao au utaifa.

Katika ujumbe uliorushwa Jumapili jioni kwenye televisheni ya taifa, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Congo alisema kwamba mzozo huu unahusu mamlaka na majeshi ya nchi zote mbili, lakini sio raia.

Kuibuka tena kwa kundi la waasi la M 23 kwenye mpaka na Rwanda na Uganda kumezorotesha uhusiano kati ya DRC na Kigali.

Nchi hizo mbili zimenyoosheana vidole zikishutumiana kuunga mkono wanamgambo wenye uhasama na upande mwingine, shutuma ambazo nchi zote zinapinga. Nchi za Afrika Mashariki zinapanga kutuma kikosi cha kikanda kupambana na makundi yenye silaha mashariki mwa DRC. Lakini kwa sasa, hakuna ratiba ya wazi ya kupelekwa kwa majeshi hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live