Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Congo DR yatishia kujitoa EAC

Tshisekedi Congo DR yatishia kujitoa EAC

Sat, 31 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo imetishia kujiondoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iwapo jumuiya hiyo itashindwa kuiwajibisha Rwanda kwa madai ya unyanyasaji katika eneo la Mashariki lililokumbwa na ghasia.

Tishio hilo lilitolewa baada ya Mahakama ya Haki ya EAC kuripotiwa kukubali kuanza kesi dhidi ya Rwanda kuhusu kuhusika kwake na ghasia mashariki mwa DR Congo.

Naibu Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Samuel Mbemba ameitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya ukatili wa Rwanda mashariki mwa DR Congo.

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limekuwa likipambana na kundi la waasi la M23 - linalodaiwa kuuungwa mkono na Rwanda ambapo taifa hilo la Rwanda limekuwa likipinga madai hayo ya Congo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live