Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Congo DR yamtaja aliyefanya jaribio la mapinduzi

MWAMBA Sac Congo DR yamtaja aliyefanya jaribio la mapinduzi

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema jaribio la Mapinduzi lililozuia mwishoni mwa wiki iliyopita liliongozwa na Mwanasiasa ambaye pia ni mwanajeshi wa zamani Christian Malanga Musumari mwenye uraia wa DR-Congo (DRC) lakini makazi yake yapo nchini Marekani akiwa na Kundi la Wanajeshi waasi.

Msemaji wa Jeshi la DRC amesema Watu 50 akiwemo mtoto wa Malanga na raia wa Marekani wamekamatwa huku Malanga akiuawa katika jaribio hilo lililoanza kwa kuvamia makazi ya viongozi wakuu wa Serikali wakiwemo Rais Felix Tshisekedi, Spika wa Bunge na Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, imedaiwa kuwa kwa takriban siku 3 nchi hiyo ilikuwa katika majaribio ya Mapinduzi ambayo Jeshi limeeleza kuwa limefanikiwa kuyazima na kurejesha hali ya utulivu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live