Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Congo: Baada ya mafuriko, hofu ya magonjwa yatanda

Mafuriko Un Msaada DRC.png Congo: Baada ya mafuriko, hofu ya magonjwa yatanda

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majimbo tisa yalikumbwa na mafuriko, watu 525,000 waliathiriwa mafuriko hayo na 27 walifariki: hii ndio ripoti rasmi ya mafuriko ya mwezi Januari huko Kongo-Brazzaville. Mamlaka inaonya juu ya athari za kiafya.

Wakati mafuriko bado yanaendelea katika baadhi ya maeneo, mamlaka inatahadharisha kuhusu madhara ya kiafya yanayoweza kutokea, hasa hatari ya mlipuko wa kipindupindu. Hakuna wagonjwa walioogunduliwa kufikia sasa.

Daktari Jean-Médard Kankou, mkurugenzi wa magonjwa na udhibiti wa magonjwa katika Wizara ya Afya, anatoa wito kwa watu kuwa waangalifu: “Kulipotokea mafuriko, kulikuwa na vyanzo kadhaa vya maji ambavyo vilichafuliwa. Kulikuwa na vijiji vizima vilivyokumbwa na mafuriko, vyoo, kila kitu kilikuwa kimejaa maji. Na kwa hivyo, baada ya mafuriko kupungua, lazima tuogope hatari ya magonjwa yanayoibuka na magonjwa yenye uwezekano wa mlipuko kama vile kipindupindu. "Tambua mapema"

"Ndio maana, katika ngazi ya Wizara ya Afya, timu zilitumwa ili kuimarisha uwezo wa wahudumu wa afya katika uchunguzi wa magonjwa na kuweza kugundua mapema magonjwa yote yenye uwezekano wa janga na hivyo kuandaa haraka majibu ikiwa hii itatokea.

"Kwa kweli, kuna ushauri wa kiafya wa kutolewa. Kwa mfano, linapokuja suala la lishe, pika chakula vizuri kabla ya kukitumia na uchemshe au kutayarisha maji kabla ya kuyatumia. Kwa sababu, kwa kweli, hofu ni hasa magonjwa haya yanayotokana na maji kama vile kipindupindu au shigellosis au hata salmonellosis. Hili ndilo tunaloliogopa zaidi ya yote. "

Chanzo: www.tanzaniaweb.live