Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Comoro yaipiga bao Tanzania viwango FIFA

Stars+comor+pic Comoro yaipiga bao Tanzania viwango FIFA

Thu, 22 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

Tanzania imeshindwa kupanda katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa mwezi Oktoba huku ikijikuta ikipitwa na Visiwa vya Comoro katika viwango hivyo.

 

Katika viwango hivyo vya ubora wa soka duniani kwa mwezi Oktoba, Tanzania imebakia katika nafasi yake ileile ya 134 ambayo ilikuwepo mwezi uliopita, ikizidiwa kete na Comoro ambayo ipo katika nafasi ya 132.

 

Kipigo cha bao 1-0 ambacho Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ilikipata kutoka kwa Burundi, Oktoba 11 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki, kinaonekana kuiponza kwa kujikuta ikiganda palepale tofauti na nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambazo nyingi zimepanda juu katika viwango hivyo.

 

Chanzo: mwanaspoti.co.tz